body-container-line-1

Entebbe na Bujumbura inakaribisha safari za ndege za uzinduzi za flydubai

By flydubai
Africa Entebbe na Bujumbura inakaribisha safari za ndege za uzinduzi za flydubai
SEP 30, 2014 LISTEN

KAMPALA, Uganda, September 30, 2014/African Press Organization (APO)/ -- Ndege za shirika la ndege la flydubai lililo na makao yake Dubai zilizozindua safari za kuenda Entebbe na Bujunbura zilitua leo na zilikaribishwa kitamaduni na saluti za mizinga ya maji na waakilishi rasmi.

Logo: http://www.photos.apo-opa.com/plog-content/images/apo/logos/flydubai.jpg

Photo : http://www.photos.apo-opa.com/index.php?level=picture&id=1297 (flydubai fleet)

Photo : http://www.photos.apo-opa.com/index.php?level=picture&id=1298 (flydubai Business Class)

Waakilishi wa flydubai (http://www.flydubai.com) waliongozwa na Hamad Obaidalla, Afisa Mkuu wa Biashara wa flydubai, na Sudhir Sreedharan, Naibu Mkuu wa Rais wa Biashara wa flydubai (GCC, Bara Dogo na Afrika), na katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Entebbe walilakiwa na Abraham Byandala, Waziri wa Uganda wa Kazi na Usafirishaji, na John Okalany, Meneja Mkuu wa Uwanja wa Ndege wa Entebbe.

Katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Bujumbura, waakilishi wa flydubai walilakiwa na Ciza Virginia, Waziri wa Usafiri, Kazi na Vifaa vya Umma, na waliburudishwa na wacheza ngoma za kitamaduni.

Kwa kuzindua safari za ndege za moja kwa moja kila siku hadi Entebbe, safari mbili za kuunganisha kila wiki za Kigali na safari tatu za kuunganisha kila wiki za Bujumbura, pamoja na utangazaji wa hivi majuzi wa njia tatu mpya nchini Tanzania, flydubai imeongeza vituo vyake barani Afrika mara mbili hadi vituo 12. Zaidi ya hayo, shirika hilo la ndege linatoa huduma za Kitengo cha Biashara na huduma za mizigo katika kila moja ya njia hivi mpya.

Akizungumzia kuhusu uzinduzi wa njia ya Entebbe, CCO wa flydibai Hamad Obaidalla alisema: "Tunafurahia safari zetu za ndege za Entebbe, moja ya kitovu kinachoongoza kibiashara barani Afrika. Tukiwa na safari za ndege za kila siku zinazotoa chaguo la kitengo cha uchumi na biashara, tutarahisisha utiririkaji wa watalii na biashara kati ya Uganda na Umoja wa Falme za Kiarabu."

Mjini Bujumbura Obaidalla alisema: "Tunaamini kwamba bioanuwai tele nchini Burundi itawavutia watalii kutoka mtandao wetu wote na kwamba zaidi ya vituo 80 tunavyoendesha vitaipa nchi hii fursa kubwa kuimarisha uhusiano wake wa biashara."

flydubai ndio shirika la ndege la kwanza la kitaifa kutoka Umoja wa Falme za Kiarabu kusafiri Rwanda na Burundi, likisisitiza ahadi yake kufungua masoko yasiyohudumiwa vya kutosha. Safari yake ya kwanza ya Kigali, Rwanda ilikuwa mnamo tarehe 27 mwezi Septemba.

flydubai inatoa safari za kuaminika na za bei nafuu hadi vituo 83 katika nchi 42. Kutoka Entebbe, Bujumbura au Kigali, abiria wanaweza kuweka nafasi za safari rahisi za kuunganisha kupitia Dubai hadi India, nchi za Ghuba na vituo mbalimbali nchini Urusi, pamoja na vituo vingine. Kitovu cha kimkakati cha shirika hilo la ndege kikiwa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Dubai, abiria pia wanaweza kunufaika kutokana na makubaliano kati ya flydubai na mashirika mengine ya ndege, na kuwapa fursa za safari za kuendelea kwa zaidi ya vituo 200.

Maelezo ya Safari za Ndege:

Entebbe, Uganda

flydubai itaendesha safari saba za ndege kila wiki kati ya Entebbe na Dubai kuanzia tarehe 28 Septemba 2014.

Jumanne, Ijumaa na Jumapili: FZ622 imepangiwa kuondoka Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Entebbe saa 7:30 usiku saa za ndani, itue katika Kituo cha 2 cha Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Dubai saa 2:05 asubuhi saa za ndani.

Jumatatu, Alhamisi na Jumamosi FZ621 imepangiwa kuondoka Kituo cha 2 cha Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Dubai saa 10:10 jioni saa za ndani, iwasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Entebbe saa 8:30 usiku saa za ndani.

Jumanne na Ijumaa: FZ624 imepangiwa kuondoka Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Entebbe saa 4:10 usiku saa za ndani, itue katika Kituo cha 2 cha Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Dubai saa 10:35 asubuhi saa za ndani.

FZ623 imepangiwa kuondoka Kituo cha 2 cha Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Dubai saa 6:20 mchana saa za ndani, iwasili Uwanja wa Kimataifa wa Entebbe saa 4:40 jioni saa za ndani.

Jumapili: FZ620 imepangiwa kuondoka Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Entebbe saa 9:15 mchana saa za ndani, itue katika Kituo cha 2 cha Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Dubai saa 3:50 usiku saa za ndani. FZ619 imepangiwa kuondoka Kituo cha 2 cha Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Dubai saa 3:55 asubuhi saa za ndani, iwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Entebbe saa 8:15 mchana saa za ndani.

Jumanne: FZ620 imepangiwa kuondoka Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Entebbe saa 7:15 mchana saa za ndani, itue katika Kituo cha 2 cha Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Dubai saa 1:50 jioni saa za ndani.

FZ619 imepangiwa kuondoka Kituo cha 2 cha Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Dubai saa 1:55 asubuhi saa ndani, iwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Entebbe saa 6:15 mchana saa za ndani.

Nauli za safari ya pande zote

Nauli ya kuenda na kurudi ya Kitengo cha Uchumi kutoka Entebbe hadi Dubai itaanzia Dola 399 za Marekani ikijumuisha mzigo wa 20kg uliokaguliwa, huku nauli ya kuenda na kurudi ya Kitengo cha Biashara itaanzia Dola 1,100 za Marekani na inajumuisha kodi zote na mzigo wa 40kg uliokaguliwa.

Bujumbura, Burundi kupitia Entebbe

flydubai itaendesha safari mbili za ndege kila wiki kati ya Bujumbura na Dubai kupitia Entebbe kuanzia tarehe 30 Septemba 2014.

Jumanne na Ijumaa: FZ624 imepangiwa kuondoka Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Bujumbura saa 12:55 jioni saa za ndani, itue katika Kituo cha 2 cha Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Dubai saa 10:35 asubuhi saa za ndani na katizo la saa moja mjini Entebbe.

FZ623 imepangiwa kuondoka Kituo cha 2 cha Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Dubai saa 6:20 mchana saa za ndani, iwasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Bujumbura saa 11:55 jioni saa za ndani na katizo la saa moja mjini Entebbe.

Nauli za safari ya pande zote

Nauli ya kuenda na kurudi ya Kitengo cha Uchumi kutoka Bujumbura hadi Dubai itaanzia Dola 399 za Marekani ikijumuisha mzigo wa 20kg uliokaguliwa, huku nauli ya kuenda na kurudi ya Kitengo cha Biashara itaanzia Dola 1,100 za Marekani na inajumuisha kodi zote na mzigo wa 40kg uliokaguliwa.

Entebbe hadi Bujumbura

flydubai itaendesha safari mbili za ndege kila wiki kati ya Entebbe na Bujumbura kuanzia tarehe 30 Septemba 2014.

Jumanne na Ijumaa: FZ623 imepangiwa kuondoka Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Entebbe saa 11:40 jioni saa za ndani, itue katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Bujumbura saa 11:55 jioni saa za ndani.

FZ624 imepangiwa kuondoka Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Bujumbura saa 6:55 jioni saa za ndani, iwasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Entebbe saa 3:10 usiku saa za ndani.

Nauli za safari ya pande zote

Nauli ya kuenda na kurudi ya Kitengo cha Uchumi kutoka Entebbe hadi Bujumbura itaanzia Dola 400 za Marekani ikijumuisha mzigo wa 20kg uliokaguliwa, huku nauli ya kuenda na kurudi ya Kitengo cha Biashara itaanzia Dola 900 za Marekani na inajumuisha kodi zote na mzigo wa 40kg uliokaguliwa.

Kigali, Rwanda kupitia Entebbe

flydubai itaendesha safari tatu za ndege kila wiki kati ya Kigali na Dubai kupitia Entebbe kuanzia tarehe 27 Septemba 2014.

Jumatatu, Alhamisi na Jumamosi: FZ622 imepangiwa kuondoka Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kigali saa 4:30 usiku saa za ndani, itue katika Kituo cha 2 cha Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Dubai saa 2:05 asubuhi saa za ndani na katizo la saa moja mjini Entebbe.

FZ621 imepangiwa kuondoka Kituo cha 2 cha Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Dubai saa 10:10 jioni saa za ndani, iwasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kigali saa 3:30 usiku saa za ndani na katizo la saa moja mjini Entebbe.

Nauli za safari ya pande zote

Nauli ya kuenda na kurudi ya Kitengo cha Uchumi kutoka Kigali hadi Dubai itaanzia Dola 399 za Marekani ikijumuisha mzigo wa 20kg uliokaguliwa, huku nauli ya kuenda na kurudi ya Kitengo cha Biashara itaanzia Dola 899 za Marekani na inajumuisha kodi zote na mzigo wa 40kg uliokaguliwa.

Tiketi za safari hizo za ndege zinaweza kununuliwa kuanzia leo kutoka tovuti ya flydubai (flydubai.com), Kituo chake cha Simu (+971) 600 54 44 45, maduka ya usafiri ya flydubai au kupitia wabia wa usafiri. Taarifa na maelezo zaidi ya huduma za shirika hili za ukodishaji gari na bima ya safiri pia zinaweza kupatikana kwenye flydubai.com.

Maelezo ya mawasiliano ya Uganda: +256-414-359-392

Maelezo ya mawasiliano ya Rwanda: +250-252-575-867

Maelezo ya mawasiliano ya Burundi: +257 79-988000

Distributed by APO (African Press Organization) on behalf of flydubai.

Media contact:

Houda Al Kaissi

Senior Press Officer

t. +971 4 603 3073

m. +971 56 683 0336

[email protected]

Kuhusu flydubai:

Shirika la ndege lenye makao yake Dubai linajikakamua kuondoa vizuizi vya usafiri na kuimarisha uhusiano kati ya tamaduni tofauti katika mtandao wake unao endelea kukua. Tangu uzinduzi wa biashara yake mnamo 2009, flydubai (http://www.flydubai.com):

• Imeunda mtandao wa vituo 83, pamoja na safari 20 mpya zilitangazwa 2014.

• Imefungua safari 53 mpya ambazo hapo awali hazikuwa na safari za moja kwa moja hadi Dubai au hazikuwa zinahudumiwa na shirika la kitaifa la Umoja wa Falme za Kiarabu kutoka Dubai.

• Imeunda msafara wa ndege 40 mpya na inasubiri kuwasilishwa kwa zaidi ya ndege 100 ifikapo mwisho wa 2023.

Zaidi ya hayo, wepesi na urahisi wa flydubai kama shirika changa la ndege umeimarisha ukuaji wa uchumi wa Dubai, kufuatana na dira ya Serikali ya Dubai, kwa kuanzisha mtiririko wa biashara na utalii katika masoko ambayo hayakuwa na huduma hizi.

Kwa maelezo zaidi kuhusu huduma za flydubai, tafadhali tembelea http://www.flydubai.com.

body-container-line